Women, children, population

Wajumbe wa Afrika wanashirikiana na UM Addis Ababa kuzingatia maendeleo ya wanawake

Darzeni za wataalamu wa kutoka Wizara za Masuala ya Kijinsia na Maendeleo ya Wanawake wakijumuika pamoja na wawakilishi wa makundi ya kieneo na kutoka mashirika ya UM, na vile vile waandishi habari, wamekusanyika hii leo Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria mkutano wa siku mbili, ulioandaliwa bia na UM/UA, kusailia maendeleo ya wanawake, kijumla, na usawa wa kijinsia katika bara la Afrika. Majadiliano haya yatalenga zaidi juuya utekelezaji wa Sera za Kijinsiya za UA, mradi ambao unahitajia kutekelezwa na mataifa husika kuendeleza usawa wa kijinsiya na maendeleo ya wanawake Afrika.~~~

Mahojiano na mwanaharakati anayepambana na UKIMWI kutoka Kenya

Hivi karibuni kulifanyika kikao maalumu kwenye Makao Makuu mjini New York kuzingatia masuala ya UKIMWI. Miongoni mwa wajumbe waliopata fursa ya kuhudhuria kikao hiki, kutokea Afrika Kusini, alikuwemo mwalimu wa skuli ya praimari katika Kenya, Jemima Nindo.

WHO inahimiza mama wazazi wanyonyeshe watoto wachanga kuwanusuru na maradhi ya utotoni

Kuanzia tarehe mosi hadi 7 Agosti nchi 120 ziada zitashiriki kwenye kampeni maalumu ya kuhamasisha mama wazazi wa kimataifa kunyonyesha watoto, hasa katika miezi sita ya kwanza baada ya kuzaliwa, kipindi ambacho imethibitika maziwa ya mama humsaidia kumpatia mtoto kinga na afya bora dhidi ya maambukizo maututi ya maradhi ya utotoni kama ugonjwa wa kupumua na kuharisha. Kampeni hii imeandaliwa na Shirika la Umoja wa Dunia Kuendeleza Unyonyeshaji (WABA). Miongoni mwa mashirika yanayojihusisha na huduma hii ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO) na pia Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) wakijumuika na wadau wengine wa kimataifa.