Fursa za msaada wa unyonyeshaji kuokoa maisha ya watoto 820,000 kila mwaka: UNICEF/ WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, na na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, wametoa wito wa kuboreshwa kwa huduma za kuwaunga mkono kina mama wanaonyonyesha kama hatua muhimu ya kuboresha usawa wa afya na kulinda haki za mama na mtoto kuishi na kustawi.