WHO

Pande kinzani Sudan acheni kushambulia wahudumu wa afya

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema lina wasiwasi mkubwa juu ya athari za machafuko nchini Sudan kwa walio na mahitaji, wahudumu wa afya na vituo vya afya.

Kuna maambuziki zaidi ya milioni 1 ya magonjwa ya zinaa kila siku :WHO

Kiwango cha kimataifa cha maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STI) kinapaswa kuwa kengele ya kuziamasha serikali, wameonya leo wataalam wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya afya wakibainisha takwimu zinazoonyesha kwamba mtu mmoja kati ya 25 leo na moja ya maradhi ya zinaa yanayotibika ambayo hutokea katika kiwango cha maambukizi zaidi ya milioni moja kwa siku.

Uchafuzi wa hali ya hewa warejesha hadhi ya baiskeli China:UNEP

Kwa muda sasa magari yamechukua nafasi ya usafiri wa baiskeli katika miji mingi ya China , lakini kutokana na ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa ambalo ni tatizo kubwa katika taifa hilo la Asia sasa baiskeli zimeanza kurejea kwa kishindo, kwa msaada mkubwa wa teknolojia na ubunifu wa karne ya 21.

Usafiri wa baiskeli una faida za kiafya isitoshe kimazingira

Mahitaji ya wasafiri ambao hutembea kwa miguu au kuendesha baiskeli, ambayo ni idadi kubwa ya watu yanapuuzwa na mataifa mengi licha ya kwamba faida za kuwekeza katika usafiri wa kundi hili zinaweza kuokoa maisha, kusaidia kulinda mazingira na kupunguza umaskini.