WHO

Uganda imewekeza dola milioni 18 kujianda dhidi ya ebola

Serikali ya Uganda na wadau wengine wamewekeza dola milioni 18 kwa ajili ya kujiandaa kukabiliana na ugonjwa wa ebola. Taarifa za shirika la afya ulimwenguni, WHO zinasema fedha hizo ni kwa ajili ya kuandaa mikakati mbali mbali ikiwemo kuwandaa watoa huduma wa afya 526 katika wilaya 14 waliopatiwa mafunzo kuhusu namna ya kuhudumia watu wanaoshukiwa kuwa na ebola huku wakijikinga.

Magonjwa yatokanyo na matumizi ya tumbaku yanagharimu dunia dola trilioni 1.4- WHO

Gharama za magonjwa yatokanayo na matumizi ya tumbaku kila mwaka ni dola trilioni 1.4 kote ulimwenguni kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la afya duniani, WHO iliyotolewa leo Mei 31 kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku.

Usikubali tumbaku ichukue pumzi yako- WHO

Kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa duniani ya kutovuta tumbaku keshokutwa Ijumaa, shirika la afya ulimwenguni, WHO  linaangazia madhara ya matumizi ya tumbaku kwa mapafu ya binadamu ikielezwa kuwa zaidi ya asilimia 40 ya vifo vihusianavyo na utumiaji wa tumbaku vilihusiana na magonjwa kama saratani, magonjwa sugu ya njia ya hewa na Kifua Kikuu.

Azimio lapitishwa Geneva kuhusu uwazi wa bei za dawa

Mkutano wa Baraza Kuu la shirika la afya duniani, WHO umefikia ukingoni leo kwa kupitisha azimio linalohusu kuboresha suala la uwazi wa masoko ya dawa, chanjo na bidhaa nyingine za afya katika jitihada za uwezekano katika kurahisisha upatikanaji bidhaa hizo. 

Dola milioni 363 zachangishwa huko Norway kukabili ukatili wa kingono kwenye mizozo

Hii leo huko Norway, jumla ya  dola milioni 363 zzimepatikana kama ahadi kutoka mataifa 21 kwa ajili ya mipango ya kukabiliana na ukatili wa kingono na kijinsia kwenye mizozo kwa mwaka 2019, 2020 na kuendelea. Fedha hizo zimepatikana wakati wa mkutano wa aina yake  ulioleta pamoja maafisa wa ngazi ya juu kutoka mataifa 90 pamoja na Umoja wa Mataifa .

Hatua mpya zatangazwa kukabili Ebola DRC, David Gressly kushika hatamu

Ikiwa ni mwezi wa tisa sasa tangu kuanza kwa mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na idadi ya wagonjwa wapya ikizidi kuongezeka katika wiki za hivi karibuni, Umoja wa Mataifa hii leo umetangaza hatua mpya za kuimarisha harakati zake dhidi ya ugonjwa huo hatari.

Algeria na Argentina zaupa kisogo ugonjwa wa malaria:WHO

Algeria na Argentina zimethibitishwa na kutambulika rasmi na shirika la afya ulimwengu WHO kuwa zimetokomeza malaria.

Muundo mpya wa sheria za dawa Afrika Magharibi wawasilishwa huko Geneva

Mkutano wa Baraza Kuu la shirika la afya ulimwenguni, WHO, ukiendelea huko Geneva, Uswisi, kamisheni ya dawa kwa nchi za Afrika Magharibi, pmoja na ile ya kimataifa kwa kushirikiana na shirika la kukabiliana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS,leo wamewasilisha mfumo bora wa sheria za dawa kwa ukanda huo wa Afrika.

Fistula yaendelea kuwa jinamizi kwa wanawake wakati wa kujifungua:UNFPA

Licha ya tahadhari na jitihada kubwa zinazofanyika kote duniani kuwanusuru, ugonjwa wa Fistula umeendelea kuwa ni jinamizi linalowaghubika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA. 

Kenya ni mfano wa mafanikio ya huduma ya afya kwa wote- Dkt. Tedros

Mkutano wa 72 wa Baraza la shirika la afya duniani, WHO umeanza leo mjini Geneva, Uswisi ukilenga kutathmini mwelekeo wa afya duniani na harakati za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan yale yahusuyo afya.