WHO

WHO yalaani shambulizi dhidi ya wahudumu wa afya Iraq

Shirika la afya duniani (WHO) limelaani vikali  shambulio la hivi karibuni dhidi ya muhudumu wa afya ambaye alishambuliwa wakati akitoa huduma kwamgonjwa mahtuti  ajuza wa miaka 70 katika Hospitali ya Azadi  iliyopo katika jimbo la Kirkuk mapema nchini Iraq tarehe 18 mwezi huu.

Ingawa hakujaripotiwa visa vipya, Ebola bado ni tishio DRC:WHO

Katika wiki tatu zilizopita hakujaripotiwa visa vipya vya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo , DRC, ambayo ni habari Njema kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO. Hata hivyo shirika hilo limeonya kwamba ugonjwa huo bado ni hatari na unaendelea kwa mwenendo wa wastani.

Wakimbizi 7,500 wa DRC waingia Uganda; UNHCR

Watu zaidi ya 7,500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) wamekimbilia Uganda kusaka hifadhi kufuatia mashambulizi mapya katika jimbo la Ituri mahsariki mwa nchi hiyo. 

Kuna ongezeko la visa vya surua kote ulimwenguni-WHO

Takwimu za Shirika la afya ulimwenguni, WHO zinaonyesha kuwa idadi ya maambukizi ya surua inaongezeka katika maeneo mabli mbali na sio changamoto ya bara moja

Sauti ya juu inaua ngoma ya msikio kwa vijana muongozo watolewa:WHO

Vijana zaidi ya bilioni moja wa umri wa kati ya miaka 12 na 35 wanajiweka katika hatari ya kupata uziwi usioweza kutibika kwa sababu ya kusikiliza sauti za juu za vitu kama muziki kwa kutumia simu za kisasa za rununu zinazoweza kufanya mambo mengi.

Ushirikiano wa kimataifa unahitajika kuhakikisha uhakika na usalama wa chakula:UN/AU

Wanasayansi, watunga sera , wawakilishi wa serikali , wakulima na walaji wanakutana kwa siku mbili mjini Adis Abba Ethiopia kwenye mkutano wa kwanza kuhusu uhakika na usalama wa chakula na jukumu lake katika maendeleo endelevu, SDG’s.

Dola milioni 43.5 zinahitajika mwaka huu kuimarisha huduma za afya Libya- WHO

Shirika la afya duniani WHO na washirika wake wametangaza ombi la dola milioni 43.5 ili kuimarisha huduma za afya nchini Libya hususan kwa watu 388,000 walioathirika na mgogoro unaoendelea nchini humo.

Uchungu wa maumivu ya mwana wamfanya mama atamani angaliugua yeye saratani

Katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani hii leo, shirika la afya ulimwenguni WHO limeangazia kwa kina saratani ya shingo ya kizazi huku ikisisitiza umuhimu wa kuchunguzwa, kupokea chanjo ya Human Papiloma Virus, HPV na kutokomeza kabisa saratani ya shingo ya kizazi.