Tangu kuibuka kwa virusi vya corona, COVID-19, duniani kote watu wamekuwa nao wakiibua na dhana mbalimbali potofu za kuhusu namna ya kujikinga au kutibu maambukizi ya virusi hivyo. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, kupitia wavuti wake pamoja na mengine, limechapisha dhana hizo potofu na kuzitolea ufafanuzi.