WHO

WHO yasema huduma za afya kwa wote zijumuishe wagonjwa wa kisukari

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa wa kisukari, shirika la afya ulimwenguni WHO linaangazia athari za kisukari kwa familia na majukumu ya wanafamilia k

Sauti -
2'48"

Huduma za afya kwa wote zijumuishe wagonjwa wa kisukari- WHO

 

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa wa kisukari, shirika la afya ulimwenguni WHO linaangazia athari za kisukari kwa familia na majukumu ya wanafamilia katika kusaidia kinga, uchunguzi na usimamizi unaotakiwa kwa ugonjwa huo ambao ulisababisha vifo vya watu milioni 1.6 mwaka 2016. 

Kampeni ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya viuavijasumu yaanza leo, elimika!

Juma hili ni wiki ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya viuavijasumu ambavyo inaelezwa kuwa matumizi yasiyo sahihi yanasababisha usugu dhidi ya vijiumbe maradhi. 

Sauti -
1'53"

Tuzingatie matumizi sahihi ya dawa kuiokoa dunia na usugu wa dawa-FAO

Juma hili ni wiki ya kuelimisha umma kuhusu matumizi ya viuavijasumu ambavyo inaelezwa kuwa matumizi yasiyo sahihi yanasababisha usugu dhidi ya vijiumbe maradhi. 

Mataifa yakishikamana, matumaini na suluhusu vinawezekana:Guterres

Kuanzia migogoro, na matatizo ya kiuchumi, hadi maradhi na mabadiliko ya tabia nchi, changamoto hizi za dunia zinahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote mshikamano imara wa kimataifa, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwaasa viongozi wa dunia kwenye kongamano la kimataifa la Amani lililofanyika leo Jumapili mjini Paris Ufaransa kuadhimisha miaka 100 tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia.

Wayemen wasimulia wanachopitia hadi kupata huduma za afya Sana’a

Nchini Yemen, Umoja wa Mataifa ukiendelea kunusuru wananchi dhidi ya mapigano yanayoendelea kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu hivi sasa, manusura wa mzozo huo wameelezea madhila wanayopata ikiwemo kusaka huduma za afya.

UN yaendelea kuhaha kunusuru wakazi wa Hudaidah nchini Yemen

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema mapigano yanayoendelea hivi sasa kwenye mji wa Hudaidah nchini Yemen yanazidi kuweka hatarini makumi ya maelfu ya watu na kuzuia shirika hilo kuwafikishia misaada ya dharura wanayohitaji

07 Oktoba 2018

Katika jarida la Umoja wa Mataifa leo Siraj Kalyango anaangazia

-Chanjo ya Ebola kwa wahudumu wa afya Uganda imeanza katika kujihadhari kabla ya shari

Sauti -
11'35"

Kuna mafanikio na changamoto katika uhakika wa chakula:SOFI

Ripoti ya mwaka 2018 ya masuala ya uhakika wa chakula na lishe duniani :SOFI 2018, imeonyesha pande mbili katika suala hili, ingawa kuna changamoto nyingi lakini pia kuna mafanikio kiasi.

Sauti -
1'57"

SOFI 2018 yaonesha pande mbili za uhakika wa chakula duniani

Baada ya maendeleo ya muda katika masuala ya uhakika wa chakula na lishe duniani, ushahidi unaonesha kuwa njaa inaendelea kuongezeka,  imesema ripoti ya mwaka huu ya hali ya uhakika wa chakula na lishe duniani, SOFI, iliyochapishwa hii leo. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.