Visa vya ugonjwa wa surua viliongezeka mwaka 2017, kutokana na milipuko isiyoisha ya ugonjwa huo katika maeneo kadhaa duniani, imesema ripoti iliochapishwa leo na shirika la afya ulimwenguni, WHO.
Kampeni ya kutoa dawa dhidi ya ugonjwa wa Malaria imezinduliwa leo jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kufuatia ongezeko la visa vya ugonjwa huo kwenye eneo hilo ambako tayari wahudumu wa afya wanahaha kukabiliana na mlipuko wa Ebola.
Taarifa ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO iliyotolewa leo mjini Baghdad Iraq imesema dawa za kuokoa maisha na vifaa tiba vingine vimewasilishwa katika hospitali ya Shirqat kama sehemu ya kuwatibu walioathiriwa na mafuriko.
Shirika la afya duniani WHO leo limetangaza kuwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inaanza kutoa dawa mpya ya majaribio. Dawa hii mkusanyiko wa dawa mbalimbali zenye lengo la kuunganisha nguvu dhidi ya virusi vya Ebola.
Shirika la afya duniani WHO limesema kazi za kupambana na mlipuko wa ugonjwa Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC baado zinaendelea licha mashambulio yaliyofanywa Ijumaa katika mji Beni nchini humo.
Katika siku ya choo duniani takwimu zoinaonyesha bado mamilioni ya watu hawana huduma hii ya msingi kote duniani , huku shirika la afya duniani WHO, likitoa wito wa kuhakikisha huduma hiyo inapatikana kwa wote endapo tunataka kutimiza malengo ya afya ifikapo 2030.
Kasi ya kupunguza visa vya malaria imesimama baada ya miaka mingi ya kupungua kwa visa hivyo kote duniani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya malaria duniani 2018 iliyotolewa leo.
Kila siku ajali za barabarani hukatili uhai wa maelfu ya watu, kuwaacha wengine na ulemavu wa maisha na kuathiri mustakhbali wa familia nyingi duniani. Na wakati wa kuchukua hatua dhidi ya zahma hiyo ni sasa limesema shirika la afya duniani, WHO.
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa wa kisukari, shirika la afya ulimwenguni WHO linaangazia athari za kisukari kwa familia na majukumu ya wanafamilia k
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa wa kisukari, shirika la afya ulimwenguni WHO linaangazia athari za kisukari kwa familia na majukumu ya wanafamilia katika kusaidia kinga, uchunguzi na usimamizi unaotakiwa kwa ugonjwa huo ambao ulisababisha vifo vya watu milioni 1.6 mwaka 2016.