WHO

Bidhaa za tumbaku lazima zidhibitiwe

Bidhaa za tumbaku zinasababisha madhara mengi sana hususani kiafya. Shirika la afya duniani WHO sasa linataka kila nchi mwanachaka kuchukua hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo kwa kuweka sheria na kuzitekeleza.

09 Machi 2018

Katika jarida la leo tunaanza na mwuongozo mpya uliyotolewa na WHO kuhusu jukumu la sheria dhidi ya bidhaa za tumbaku. Tunaangazia pia jinsi Tanzania imejipanga kufanikisha maendeleo ya uchumi kutokana na viwanda. Pata pia makala ya midundo na uchambuzi wa neno la wiki. 

Sauti -
11'27"

Katu hatukubali tumbaku iendelee kuua binadamu

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa mwuongozo mpya kuhusu ujukumu la sheria dhidi ya bidhaa za tumbaku na kuonyesha jinsi zinavyoweza kupunguza mahitaji, kuokoa maisha na kupunguza gharama za huduma ya afya katika kutibu maradhi yatokanayo na bidhaa za tumbaku.

Sauti -
2'12"

Vifo milioni 7 kila mwaka vitokanavyo na tumbaku havistahiki: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO leo limetoa mwuongozo mpya kuhusu ujukumu la sheria dhidi ya bidhaa za tumbaku na kuonyesha jinsi zinavyoweza kupunguza mahitaji, kuokoa maisha na kupunguza gharama za huduma ya afya katika kutibu maradhi yatokanayo na bidhaa za tumbaku.

Sheria itasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya viuavijasumu: Dr Mbindyo

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema matumizi mabaya na ya kupindukia ya viuavijasumu au antibiotic yana athari kubwa sio tu kwa afya ya binadamu na wanyama bali pia katika uchumi. Sasa shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la afya ya mifugo OIE wanazichagiza nchi kuchukua hatua ili kuepuka athari hizo kwa kudhibiti matumizi ya dawa za viuavijasumu kwa binadamu na wanyama.

Sauti -
3'49"