Viongozi wa nchi na wakuu wa serikali leo wamepitisha azimio la kisiasa lenye lengo la kuchagiza hatua dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, au TB unaosababisha vifo vya watu milioni 1.6 kila mwaka.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto, UNICEF likishirikiana na washirika wao linasema limeorodhesha watoto 155 ambao wamepoteza wazazi wao au waliachwabila mlezi kutokana na mlipuko ugonjwa wa Ebola uliotokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Nchini Uganda, shirika la afya ulimwenguni, WHO kwa ushirikiana na wizara ya afya wanaendelea na maandalizi ya kuwapatia chanjo wahudmu wa afya na wananchi walio hatarini kukumbwa na ugonjwa wa Ebola iwapo itahitajika kufanya hivyo.
Ripoti mpya ya shirika la afya ulimwenguni WHO kuhusu hali ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani, TB inasema kuwa idadi ya watu waliougua kifua kikuu au kufariki dunia mwaka jana ilikuwa ni ndogo ingawa bado mataifa mengi hayachukui hatua za kutosha kuweza kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka wa 2030.
Umoja wa Mataifa nchini Yemen uko kwenye harakati za kuwezesha kufunguliwa kwa safari za ndege ili kuwezesha wagonjwa mahututi kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu ya magonjwa ambayo hayawezi kutibiwa nchini humo.
Kuendelea kwa vita nchini Yemen kumezidisha machungu kwa wagonjwa wa figo ambao hivi sasa wanalazimika kusafiri muda mrefu kusaka huduma za kuondoa maji yanayojaa mwilini kama njia ya kusafisha figo zao.
Zaidi ya wagonjwa wapya milioni 18 wa saratani wameripotiwa mwaka huu wa 2018 huku watu wengine zaidi ya milioni 9.5 wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa huo katika kipindi hicho.