WHO

Tusipopima na kutibu haraka homa ya ini tutakuwa na mtihani mkubwa -WHO

Mataifa yote duniani yametolewa wito wa  kuongeza  huduma za haraka za upimaji  na matibabu dhidi ya homa ya ini ili kufikia malengo ya afya yaliyokubaliwa duniani.

Mlipuko wa Ebola kwaheri DRC: Tedros

Shirika la afya ulimwenguni WHO, kwa ushirikiano na wizara ya afya ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo   DRC, leo wametangaza rasmi kumalizika kwa  mlipuko wa Ebola katika jimo la Equateur nchini humo  baada ya jitihada za zaidi ya miezi miwili za kuudhibiti ugonjwa huo.

Hatua zimepigwa lakini safari bado ni ndefu katika vita dhidi ya ukimwi:WHO

Kongamano la 22 la kimataifa kuhusu ukiwmi limefunguliwa rasmi hii leo mjini Amsterdam Uholanzi likihimiza jitihada za kukabiliana na maambukizi mapya hususan kwa vijana barubaru.

Ukata wafungasha virago wahudumu wa afya Iraq

Ukosefu wa fedha unatishia kufungwa kwa vituo muhimu vya afya nchini Iraq na hivyo kuacha mamilioni  ya watu bila fursa ya kupata dawa muhimu na huduma ya afya.

Dawa za kuua vijiumbe maradhi bado zinauzwa kiholela- Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo imesema licha ya hatua za kudhibiti usugu wa dawa dhidi ya vijiumbe maradhi, AMR, bado kuna changamoto kubwa katika utekelezaji wa makubaliano na hivyo hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa.

Chondechonde ruhusuni huduma za afya ziwafikie wahitaji kusini mwa Syria- WHO

Shirika la afya duniani, WHO limetoa wito kwa ulinzi wa vituo vya huduma za afya huko kusini mwa Syria sambamba na kutoa fursa zaidi kwa watoa misaada kuingia eneo hilo.

Hali ya afya kwa maelfu Hodeidah, Yemen ni mtihani mkubwa

Hali ya afya Hodeidah, ambayo hata kabla ya machafuko ilikuwa tete sasa iko njia panda limeonya leo shirika la afya duniani WHO.