wazee

Janga la COVID-19 limeongeza ukatili dhidi ya wazee: mtaalam wa UN aonya

Wakati mitazamo ya zamani kuhusu uzee tayari inadhoofisha uhuru wa wazee katika kufanya uchaguzi na maamuzi yao wenyewe, janga la COVID-19 limeleta zahma zaidi, dhuluma na kutelekezwa dhidi watu hao, ameonya leo mtaalam huru wa  haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, katika ujumbe wake kuhusu Ulimwengu siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhudu ukatili dhidi ya wazee.

Wakimbizi wazee Afrika hatarini zaidi kuathiriwa na COVID-19

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kwamba zaidi ya wazee 500,000 barani Afrika wako hatarini kupata viru

Sauti -
1'42"

Wazee wakimbizi takriban 500,000 hatarini kupata COVID-19 Afrika:UNHCR 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeonya kwamba zaidi ya wazee 500,000 barani Afrika wako hatarini kupata virusi vya corona au COVID-19 endapo hatua madhubuti hazitachukuliwe sasa na wadau wote kuwalinda.

Wazee katika jamii wanabeba mzigo mzito kufuatia vita Ukraine

Vita vinavyoendelea Mashariki mwa Ukraine vimeongeza madhila kwa maelfu ya wazee na sasa janga la corona au COVID-19 imekuwa ni kama msumari wa moto juu ya kidonda.

Sauti -
2'16"

Vita vinavyoendelea Mashariki mwa Ukraine ni mslaba mzito kwa wazee:OCHA 

Vita vinavyoendelea Mashariki mwa Ukraine vimeongeza madhila kwa maelfu ya wazee na sasa janga la corona au COVID-19 imekuwa ni kama msumari wa moto juu ya kidonda. Mfuko wa msaada wa kibinadamu wa Ukraine unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa ndio mkombozi pekee kwa wazee hawa. 

Ukatili wa maneno na mtandaoni unakiuka haki za wazee lazima ukomeshwe:UN

Ikiwa leo ni siku ya uelimishaji kuhusu ukatili dhidi ya wazee duniani Umoja wa Mataifa umesema ukatili wanaofanyiwa wazee kwa maneno au mtandaoni unakiuka haki za binadamu za watu wa kundi hilo na ni lazima ukomeshwe. 

Janga la COVID-19 ni jinamizi kwa wazee-Guterres

Janga la virusi vya corona au COVID-19 linasababisha hofu isiyoelezeka na madhila kwa wazee kote ulimwenguni.

Sheria ya kuwalinda wazee yatoa matumaini kwa wazee kukabiliana na madhila wanayoyapitia Tanzania

Nchini Tanzania kuna Sera ya wazee iliyotungwa mwaka 2003 lakini hadi sasa haijatungwa sheria ya kusimamia utekelezaji wa sera hiyo.Wazee wanasema kuwa sheria ya kuwalinda ndio muarobaoni wa changamoto za maisha wanazokabiliana nayo hasa kiuchumi kwani wanapoishiwa nguvu za uzalishaji, hukosa mah

Sauti -
4'11"

Msumbiji ilinde wazee dhidi ya ukatili hususan wakati wa dharura- Mtaalam huru UN

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa aliyeko ziarani Msumbiji amepongeza serikali ya nchi hiyo kwa juhudi zake na dhamira ya kuweka sera na sheria za kuhakikisha wazee wanafurahia haki zao huku akisisitiza utekelezaji unahitajika. Akizingatia hali ya dharura ya sasa kutokana na vimbunga Idai na Kenneth, mtaalamu huyo ametoa wito kwa mamlaka kuhakikisha wazee wanalindwa kutokana na ukatili na unyanyasaji.

PADI Ruvuma nchini Tanzania yasaidia utekelezaji wa lengo namba 10 la SDGs

Shirika la kiraia la PADI lenye lengo la kusaidia watu maskini na wenye ulemavu, limekuwa chachu ya maendeleo kwa wazee kwenye manispaa ya Songea mkoani Ruvuma nchini Tanzania.

Sauti -
3'49"