Chuja:

wayahudi

Ua la waridi lililowekwa kwenye njia ya reli katika Makumbusho ya Auschwitz-Birkenau, nchini Poland.
Unsplash/Albert Laurence

Ni jukumu la kila mtu kuzungumza na kuendeleza kumbukumbu ya Holocaust: Katibu Mkuu wa UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumamosi ya leo akishiriki katika sinagogi ya Park East jijini New York Marekani katika maadhimisho ya kusherehekea ukombozi wa kambi ya mateso ya Auschwitz; amesema ni jukumu la kila mmoja kuenzi kumbukumbu za waliofariki katika mauaji ya maangamizi makubwa au Holocaust dhidi ya wayahudi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akiweka shada la m aua huko Christchurch New Zealand kuenzi waathirika wa shambulio la Machi mwaka huu.
UN /Mark Garten

Siku ya kimataifa ya waathirika wa matendo ya vurugu yanayotokana na dini au imani yaadhimishwa kwa mara ya kwanza.

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuadhimisha waathirika wa matendo ya vurugu yanayotokana na dini au imani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ulimwengu unapaswa kupinga na kukataa wale ambao kwa mabavu na kwa uongo wanashawishi kujenga imani potofu, kuchochea mgawanyiko na kueneza hofu na chuki. 

Sauti
1'43"
UN

Natumia uelewa wangu kuhusu mauaji ya halaiki kuepusha yasiyotokee tena- Mwanafunzi Tanzania

Miaka 74 tangu kukombolewa kwa kambi ya mateso na mauaji ya wayahudi milioni Sita huko  Auschwitz-Birkenau, nchini Poland yaliyofanywa na manazi wa Ujerumani, bado kuna ubaguzi kwa misingi mbalimbali iwe ya kidini au kikabila. Hali hii  hutia sana wasiwasi Umoja wa Mataifa ambao uliamua siyo tu kutenga siku ya kimataifa ya kumbukizi ya mauaji hayo ya halaiki dhidi ya wayahudi kama fursa ya kukumbuka na kutathmini, bali pia kuwa na programu maalum ya kuelimisha jamii juu ya madhila ya mauaji ya aina hiyo na viashiria vyake ili kuepusha yasitokee tena.

Sauti
4'5"