Wau

Kiu ya amani Sudan Kusini ni dhahiri- Shearer

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kusini, David Shearer, ametembelea eneo la Bahr El Ghazal nchini humo ambako amekuwa na mazungumzo na viongozi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa mkataba wa amani, kusaidia wakimbizi wa ndani kurejea kwa hiyari katika maeneo yao na pia kuhusu suala la usalama katika ukanda huo.

20 Februari 2019

Ripoti ya Umoja wa Mataifa yasisitiza kuwa vita na ukwepaji sheria lazima vikome Sudan Kusini. Pia baadhi ya wakimbizi wa ndani wameanza kunufaika na mkataba wa amani wanasema kutokana na mkataba wa amani, angalau hali ya usalama imetengamaa.

Sauti -
13'34"

Kutokana na mkataba wa amani, angalau hali ya usalama imetengamaa-Wakimbizi Sudan Kusini

Baada ya kuyakimbia mapigano katika Kijiji chao cha Ngovu na wakajificha karibu na kituo cha ulinzi wa raia cha Umoja wa Mataifa huko Wau, Sudan Kusini, Regina na Mayige Lina James sasa wamereja katika Kijiji chao wakiwa na matumaini kuwa makubaliano ya amani yatawaruhusu kuanza maisha yao upya. 

Kampeni ya usafi Wau yahamasisha wakimbizi kurejea nyumbani:UNMISS 

Kampeni kubwa inafanyika jimboni Wau nchini Sudan Kusini  kwa ushirikiano wa Umoja wa Mataifa, serikali na wenyeji ili kujenga mazingira salama na stahiki na hatimaye familia za wakimbizi wa ndani zilizotawanywa na miaka ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ziweze kurejea nyumbani.