Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani hii leo Naibu Katibu Mkuu wa chombo hicho Amina J. Mohammed ameongoza tukio la maadhimisho ya siku ya watu wa asili, ambayo maudhui yalikuwa lugha za asili.
Kufuatia ukweli ya kwamba lugha 600 za kiasili hupotea kila baada ya wiki mbili, Umoja wa Mataifa hii leo kwenye makao yake makuu mjini New York, Marekani umezindua rasmi mwaka wa kimataifa wa lugha hizo.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Miroslav Lajčák amefungua jukwaa la watu wa jamii ya asili akisema katu isisahaulike kuwa Umoja wa Mataifa ni kwa ajili ya watu wote ikiwemo watu wa asili.