Msingi wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ni utambuzi ya kwamba maendeleo yasiyotambua watu kama wanufaika wakuu wa hatua hiyo si maendeleo bali uchumi usio na manufaa.
Kikao cha 17 cha jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili kimeanza leo kwenye makao makuu ya umoja huo, jijini New York, Marekani. Mada kuu katika mkutano huo ni haki za ardhi, maeneo na rasilimali kwa watu hao wa jamii za asili.