watoto

Miaka mitano ya mzozo Ukraine, zaidi ya shule 750 zimesambaratishwa- UNICEF

Nchini Ukraine, mashambulizi dhidi ya maeneo ya shule yameongezeka mara nne katika robo ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, imesema taarifa iliyotolewa leo huko Kiev, Ukraine na New York, Marekani ikiongeza kuwa matukio hayo yamesababisha kiwewe kwa wanafunzi na kuwatia hatarini kupata majeraha au kuuawa.

Watoto waachiliwa huru Nigeria, UNICEF yajipanga kuwawezesha kumudu maisha ya uraiani

Watoto takriban 900 waliokuwa wakishikiliwa na makundi mbalimbali yenye silaha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wameachiliwa huru na makundi mbalimbali yenye silaha na kufanya idadi ya walioachiliwa na makundi hayo tangu mwaka 2017 kufikia zaidi ya 1700. Amina Hassan na taarifa zaidi.

Sauti -
2'1"

Takriban watoto 900 waachiliwa huru na makundi yenye silaha Nigeria:

Watoto takriban 900 waliokuwa wakishikiliwa na makundi mbalimbali yenye silaha Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wameachiliwa huru na makundi mbalimbali yenye silaha na kufanya idadi ya walioachiliwa na makundi hayo tangu mwaka 2017 kufikia zaidi ya 1700. 

Watoto 12 wauawa Syria katika wiki mbili zilizopita

Takribani watoto 12 wameuawa kaskazini-magharibi mwa Syria tangu tarehe 20 mwezi uliopita wakati huu ambapo ghasia zinazidi kwenye ukanda ambao haupaswi kuwa na mapigano.

Watoto 5 wanyongwa Iran na Saudi Arabia,  UNICEF yapaza sauti

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya ripoti za mara kwa mara za kuuawa kwa watoto kwenye mataifa ya kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, MENA.