watoto

WFP yaipiga jeki Tajikistan ili iondokane na njaa 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP, limezindua mchakato wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa chakula nchini Tajikistan ikiwa ni  sehemu ya mkakati wa miaka mitano wa nchi hiyo wa kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2024.

Taarifa za wahamiaji kutelekezwa jangwani zinasikitisha: IOM

Si haki kwa wahamiaji ambao ni pamoja na kina mama wajawazito na watoto kutelekezwa peke yao bila chakula wala maji au kutarajiwa wataweza kutembea kwa miguu maili kadha katika joto kali wakitafuta usalama jangwani.

Madhila yanayowakabili raia Hodeidah Yemen hayaelezeki:Grande

Wiki moja baada ya mapigano kuanza kwenye uwanja wa ndege katika mji wa bandari wa Hodeidah, maelfu ya raia wamesalia katika hatari kubwa hali ambayo inalitia hofu kubwa shirikala Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.

Watoto hawapaswi kutenganishwa na familia licha ya hali ya uhamiaji-UNICEF

Taarifa ya kwamba watoto wakiwemo wachanga wanatenganishwa na wazazi wao wakati wanatafuta usalama nchini Marekani zinaumiza moyo, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

Watoto milioni 30 waliotawanywa na vita wanahitaji kulindwa, na pia suluhu ya kudumu:UNICEF

Takribani watoto milioni 30 waliotawanywa na vita duniani wanahitaji ulinzi sasa na suluhu endelevu na ya kudumu kwa ajili ya mustakbali wao.

Haki za watoto wakimbizi na wahamiaji ni suala la kanuni: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametetea haki za watoto wakimbizi na wahamiaji akisema ni suala la kuzingatia kanuni za haki za binadamu bila kuisota kidole Marekani.

Watoto wengine zaidi ya 200 waachiliwa na waasi Sudan Kusini:UNICEF

Kwa mara ya tatu mwaka huu watoto wengine zaidi ya 200 wameachiiliwa Alhamisi na makundi ya waasi nchini Sudan Kusini.

Vijana wanahitaji mazingira salama kazini :ILO

Wafanyakazi vijana kote duniani ndio walio katika hatari zaidi ya kujeruhuwa kazini kutokana na kemikali au madawa ya aina nyingine kwa sababu ya maendeleo yao ya kimwili na kiakili. 

Chanjo inaokoa na kuboresha maisha: WHO

Wiki ya chanjo duniani kwa mwaka 2018 imeng’oa nanga leo  Aprili 24 na itakamilika Aprili 30 .

Iran acheni kuwanyonga watoto mnakiuka sheria za kimataifa: Zeid

Kamisha Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein leo ameitaka serikali ya Iran kuheshimu, kuzinhatia sheria za kimataifa na kukomesha mara moja unyongaji wote wa watu waliohukumiwa kifo kwa makossa waliyoyatenda wakiwa watoto, barubaru au vijana wadogo.