watoto

Mzozo wa Syria ukikaribia kutimu miaka 8, UNICEF yapigia chepuo mahitaji ya watoto

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF Henrietta Fore amehitimisha ziara yake ya siku 5 nchini Syria akisema suala la kufikia watoto wote kwenye taifa hilo lililogubikwa na vita kwa takribani miaka 8 sasa linasalia jambo muhimu.

UNICEF yaingiwa hofu juu ya hali ya watoto wahamiaji mpakani mwa Mexico na Marekani

UNICEF ina wasiwasi mkubwa juu ya usalama na ustawi wa zaidi ya watoto wahamiaji 1,000 walioko kwenye msafara huko Mexico au wakisubiri huko eneo la mpakani la Tijuana wakati huu ambapo madai yao ya kusaka hifadhi yakishughulikiwa na mamlaka za Marekani.

Pengo la ufadhili linahatarisha maisha ya watoto milioni 1 Mashariki ya kati:UNICEF

Takribani watoto milioni moja wa eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wako hatarini wakati huu ambapo msimu wa baridi kali unanyemelea eneo hilo. Kutokana na hali hiyo ambayo watoto hao wanahitaji msaada wa haraka, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ombi la dola milioni 33 ili kufikisha misaada.

Mahabusu kwa waoomba hifadhi Libya zisite:UNHCR

Ikiwa leo ni mwaka mmoja tangu shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lianze operesheni ya kuokoa maisha ya kuwahamisha kutoka Libya maelfu ya wakimbizi na waoomba hifadhi, jumla ya watu 25000 wameshahamishwa wengi walikuwa mahabusu au kushikiliwa kwenye vituo maalumu.

Mabaraza ya watoto nchini Tanzania yanasongesha haki za watoto

Ikiwa leo ni siku ya mtoto duniani, maudhui yakiwa sambaza rangi  ya buluu ili kutetea haki za mtoto, mkoani Mwanza nchini Tanzania watoto nao wameshika hatamu kuhakikisha haki  hizo zinapatiwa kipaumbele.

Vaa nguo ya buluu tarehe 20 Novemba kuunga mkono kampeni ya watoto

Kuelekea siku ya watoto duniani tarehe 20 mwezi huu wa Novemba, mtoto muigizaji Millie Bobby Brown ameungana na mabalozi wema wa shirika la kuhudumia watoto duniani,  UNICEF kutumia video mahsusi kupigia chepuo kampeni ya kusongesha haki za watoto duniani. 

Baada ya siku sita misafara ya misaada yakamilika Rukban Syria:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, washirika wa Umoja wa Mataifa na chama cha msalaba mwekundu nchini Syria, wamekamilisha misafara ya siku sita ya misaada ya kibinadamu kwenye kambi ya Rukban iliyoko Kusini Mashariki mwa Syria karibu na mpaka wa Jordan.

Chonde chonde Saudia sitisheni hukumu ya kifo kwa watoto:UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Saudi Arabia kusitisha mara moja utekelezaji wa hukumu ya kifo kwa watu sita waliohukumiwa kufa kwa madai ya kufanya uhalifu walipokuwa na umri wa chini ya miaka 18.

Zaidi ya watoto 2000 walio kwenye msafara Amerika ya Kati wanahitaji msaada- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto la UNICEF limeonya kuwa takriban watoto 2,300 walio katika msafara wa maandamano ya watu ambao sasa uko kusini mwa Mexico wanahitaji ulinzi na huduma muhimu kama vile afya, maji safi na huduma za kujisafi.

Sitisheni mapigano ili kunusuru maisha ya watoto Yemen :UN

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa  Mataifa, OHCHR pamoja  na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wametoa wito kwa pande kinzani katika migogoro ya kivita inayoendelea nchini Yemen kusitisha mapigano ili kuokoa maisha ya raia wasiokuwa na hatiawakiwemo na watoto .