Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameihimiza serikali ya Nicaragua ikomeshe ukandamizaji kufuatia siku 100 za maandamano ambapo watu takriban 317 wameuawa ilhali wengine 1,830 wamejeruhiwa.
Wataalamu wawili huru wa Umoja wa mataifa wa masuala ya haki za binadamu wamekaribisha hatua ya kutomwaga damu Zimbamwe wakati wa kuhamisha madaraka kutoka kwa RaisRobert Mugabe ,na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono hatua hiyo kwa kuondoa vikwazo.