Wataalam wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Saudi Arabia iwaachilie huru mara moja wanawake wanaharakati waliowekwa ndani katika msako uliofanyika nchini humo hivi karibuni, wakati huu ambapo taifa hilo limeondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.