Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

wanyama

Kuku ni mali inayoshikiliwa sana kiuchumi na lishe katika afrika ya vijijini na mara nyingi husimamiwa na wanawake.
© FAO/Believe Nyakudjara

Jukwaa la Kimataifa la FAO kuhusu vyakula vya wanyama na udhibiti wake

Jukwaa hili la siku mbili lilionaza leo Novemba 14 linaangazia sekta ambayo inazalisha zaidi ya dola bilioni 400 katika mauzo ya biashara ya kila mwaka na kuzalisha zaidi ya tani bilioni moja za malisho ya:

·        Mifugo,

·        Mchango muhimu kwa afya ya Wanyama

·        Lishe ya binadamu na

·        Uendelevu wa mazingira.

Dungusi kakati ni jibu la njaa- FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema majani na matunda ya dungusi kakati ni suluhu ya ukosefu wa chakula kwa binadamu na mifugo katika maeneo yenye  ukame.

Ni kwa mantiki hiyo FAO tayari imekutanisha wataalamu ili kubonga bongo kusaidia wakulima na watunga sera juu ya jinsi ya kutumia vema tunda hilo lenye rangi nyekundu ambalo mara nyingi hupuuzwa.