Shirika la Umoja wa Mataifala Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Uganda limesema linajitahidi kuhakikisha kwamba hatua ya serilkali ya kuyasimamisha mashirika ya misaada yasiyo ya kiserikali 208 nchini humo kwa kutokidhi vigezo vya sheria kuhudumia wakimbizi , haiathiri utoaji wa huduma kwa wakimbizi hao.