wakimbizi

Jumuiya ya kimataifa inawajibika kimaadili kusaidia wasyria-Guterres

Serikali kote ulimwenguni zinawajibika kimaadili kusaidia wasyria kwa ajili ya mustakabali bora na hatimaye kuweka kikomo mzozo wa miaka minane, amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kupitia taarifa yake iliyotolewa Ijumaa.

Zaidi ya Wavenezuela 5,000 wapata makazi mapya Brazil:UNHCR

Zaidi ya raia 5,000 wa Venezuela wamehamishwa kutoka katika jimbo la Kaskazini mwa Barazil la Roraima na kupelekwa katika majimbo mengine 17, ikiwa ni asante kwa mpango wa ubunifu wa uhamisho wa ndani unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR , asasi za kiraia na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa lile la uhamiaji IOM, la idadi ya watu duniani UNFPA na la mpango wa maendeleo UNDP.

Mazingira wanayoishi Wasyria yanasikitisha , UN yahitaji dola bilioni 8.8 kuwanusuru.

Umoja wa Mataifa umetoa ombi la dola bilioni 8.8 kwa ajili ya kuwasaidia mamilioni ya Wasyria wanoishi katika mazingira magumu nje na ndani ya nchi hiyo iliyoghubikwa na machafuko pamoja na jamii zinazowahifadhi.

Libya tuko tayari kuwasaidia mbinu mbadala ya kushikilia wasaka hifadhi - UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema liko tayari kusaidia Libya kuandaa maeneo mbadala ya kushikilia wasaka hifadhi badala ya vituo vya korokoroni ambavyo vimekuwa kero na kusababisha kiwewe miongoni mwa wasaka hifadhi hao.