wakimbizi

Nalima na kushona cherahani kujikomboa mimi na wanawake wenzangu: Mkimbizi Felicitee

Mkimbizi Felicitee Anibati kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo ambaye kwa sasa anaishi katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu, ni mama, mkulima na mjasiriamali mwenye mafanikio ambaye sasa anawasaidia wanawake wenzie kufika alipo yeye.

Asante UNHCR kwa kunipa fursa ya kipekee maishani: Mkimbizi Saber 

Programu ya kimataifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ushirikiano na serikali ya Italia ya kuwasaidia wakimbizi kupata elimu ya juu nchini Italia imekuwa ni ngazi ya kufikia matarajio ya mkimbizi Saber ambaye kwa miaka 19 alikuwa akiishi kwenye kambi ya wakimbizi nchini Ethiopia.

Mashindano ya Olympiki ya walemavu yang'oa nanga Tokyo  wakimbizi  hawakuachwa nyuma: UNHCR

Mashindano ya kimataifa ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu yameanza rasmi hii leo mjini Tokyo Japani yakihusisha washiriki wa michezo mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia wakiwemo wakimbizi.

Wakimbizi wa Rohingya Coxi’s Bazar waanza kupokea chanjo ya COVID-19:UNHCR (OVERNIGHT)

Maelfu ya wakimbizi wa Rohingya kwenye kambi ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh sasa wameanza kupokea chanjo dhidi ya COVID-19 kama sehemu ya mkakati mkubwa wa kitaifa wa kudhibiti kusambaa kwa virusi vya gonjwa hilo.

Mapenzi ya ufumaji yampa riziki Libya mkimbizi kutoka Syria

Kutana na mkimbizi Fidaa kutoka Syria ambaye pamoja na familia yake walifungasha virago miaka minane iliyopita wakikimbia mapigano na kupata hifadhi Libya. Sasa changamoto za janga la corona au COVID-19 zimemlazimisha kurejea mapenzi ya zamani ya ufumaji ili kupata mkate wa kila siku wa familia yake.

Nakuombea ushinde ili tusherehekee sote: Mzazi wa mwanariadha mkimbizi Tokyo 

Wanamichezo wakimbizi wanaoshiriki katika michuano ya Olympiki Tokyo Japan wametumiwa salamu za heri na familia zao zilizoko katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.  Hiyo ni kwa mujibu wa video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Mkataba wa wakimbizi watimiza miaka 70 leo 

Ikiwa leo ni miaka 70 tangu kusainiwa kwa mkataba wa kimataifa wa wakimbizi mwaka 1951, wanufaika wa nyaraka hiyo wanashukuru kwa kuwa bila nyaraka hiyo maisha yao yangalikuwa ya tabu .

Mungu anatuambia tusipoteze matumaini nami sijapoteza yangu: Mkimbizi Mihret

Mihret Gerezgiher mwenye umri wa miaka 25 ni mkimbizi kutoka Ethiopia lakini sasa anaishi katika makazi  ya wakimbizi  ya Tunaydbah Mashariki mwa Sudan. Alilazimika kukimbia na nguo alizovaa tu na kuacha kila kitu machafuko yaliposhika kasi jimboni kwake Tigray Novemba 2020, unyama alioushuhudia anasema bado unampa jinamizi kila alalapo

Sijui nani atanipatia hakikisho la maisha ya baadaye ya wanangu- Mkazi Gaza

Mashambulizi ya mara kwa mara katika Ukanda wa Gaza, Palestina yamesababisha mama wa watoto watatu wa kiume kuwaza na kuwazua kuhusu mustakabli wa watoto hao ambao kila uchao ndoto zao zinakumbwa na sintofahamu.

UNHCR yaitisha mkutano na wadau kuijadili suluhu ya Venezuela

Venezuela, moja kati ya Mataifa ambayo wananchi wake wanalikimbia kwa wingi takwimu kwenda kuomba hifadhi mataifa mengine ambapo takwimu za hivi karibuni zinaonesha takribani robo ya wananchi wake wamekimbia hali ambayo imeshafanya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano hii leo kutafuta suluhu ya kudumu. Tuungane na Leah Mushi kwa undani wa taarifa hii