24 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na Mwanaisha Ulenge ni Mwanamke Mwanasayansi Mhandisi, Mbunge nchini Tanzania vilevile Mjumbe wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU) na hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Anold Kayanda alipata fursa ya kujadiliana naye kuhusu nafasi ya mwanamke katika sayansi na teknolojia.