Chuja:

Wakimbi na wahamiaji

09 Desemba 2021

Karibu kusikiliza jarida, mwenyeji wako ni Flora Nducha anayekujuza kwa undani kuhusu. 

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imesema janga la COVID-19 limeleta hali mbaya zaidi kwa watoto kuwahi kushuhudiwa katika historia yake ya miaka 75 nakuzitaka nchi kuongeza juhudi kuwanusuru watoto.

Sauti
13'15"

July 01, 2021

Katita Jarida hii leo tunakujuza kuhusu ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inayoonesha usaidizi wa kifedha kwa jamii ili kukabili umaskini uliosababishwa na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 ulikuwa mkubwa zaidi kwa wananchi wa nchi za kipato cha juu huku wale wa nchi maskini wakiambulia kidogo sana au hata patupu. Pia utasikia kuhusu matumaini ya wakimbizi nchini DRC na Somalia. 

Sauti
12'46"

June 24, 2021

Katika Jarida hii leo utasikia Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, David Beasley, ameiomba dunia kutoipa kisogo Masdagascar ambako maelfu ya watu wanakabiliwa na njaa kali na badala yake kujitoa na kuchukua hatua haraka baada ya kushuhudia mgogoro mkubwa usioonekana wa njaa unaoendelea Kusini mwa nchi hiyo  na kuathiri jamii nzima. 

Pia utasikia kuhusu wasiwasi wa wazazi nchini Palestina juu ya maisha ya baadae ya watoto wao ikiwa nchi yae itaendelea na machafuko. 

Sauti
12'11"
Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi akichora ujumbe wa Amani akiwa ziarani nchini Colombia
© UNHCR/Santiago Escobar-Jarami

Asanteni Amerika ya Kusini kwa kuwafanya wakimbizi ni sehemu ya wananchi wenu 

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya wiki moja ya kutembelea nchi zilizoko Amerika ya Kusini na kuzishukuru nchi hizo kwa kazi kubwa ya kuhifadhi wakimbizi ambapo takwimu zinaonesha wamehifadhi zaidi ya robo ya wakimbizi wote duniani.

Sauti
1'51"

21 Juni 2021

Leo katika Jarida Assumpta Massoi anakuletea

-Kamishina mkuu wa haki za binadamu Michelle Bachelet aitaka dunia kutoacha ukiukwaji wa haki za binadamu uendelee

-Shirika la afya la Umoja wa Msataifa WHO limesema milipuko ya Ebola Afrika Magharibi mwaka 2014-2016 imetoa funzo kubwa la kukabiliana na magonjwa na mchakato wa kusambaza chanjo

-Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO leo limetoa ripoti ya utafiti ikiangazia mifumo ya chakula ya watu wa asili na athari za kutoweka kwa mifumo hiyo kwa dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Sauti
11'3"
WFP/Jonathan Dumont

Ajira kwa wakimbizi wazee ni adimu zaidi

Ili kuweza kuishi maisha ya kistaarabu na staha niwajibu kuwa na shughuli ya kukuingizia kipato. Mzee Agapito Andrade mkimbizi raia wa Colombia anayeishi nchini Equador imekuwa ngumu kupata ajira na hivyo hata mlo kwake umekuwa tabu huku janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 likiongeza ugumu maradufu kupata ajira. Taarifa Zaidi tuungane na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta Massoi)

Wakimbizi kutoka Côte d’Ivoire wakisubiri kuandikishwa huko Liberia Oktoba 2020.
© UNHCR/Roland Tuley

Idadi ya watu wanaohama kwa kulazimishwa yavuka milioni 80, COVID-19 nayo ikizidisha machungu

Wakati picha kamili ya mwaka 2020 bado haijafahamika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linakadiria kuwa uhamishaji wa kulazimishwa ulimwenguni au ufurushwaji ulizidi milioni 80 katikati ya mwaka, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi kuhusu mwenendo wa uhamishaji wa kulazimishwa ulimwenguni.