Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Flora Nducha
-Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibindamu na masula ya dharura OCHA yatoa shukrani zake kwa wahudumu wa kibinadamu kokote waliko katika kuokoa maisha.
Wahudumu wa kibinadamu ni wanawake na wanaume mashujaa ambao hufikisha msaada wa kuokoa maisha kama malazi, huduma muhimu za afya, chakula, maji na huduma za usafi kwa watu wasiojiweza na walio hatarini, hivyo wanastahili kuheshimiwa na kupongezwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limelaani vikali mauaji ya wahudumu watatu wa misaada ya kibinadamu wa shirika hilo yaliyofanyika Jumapili kwenye jimbo la Equatoria ya Kati nchini Sudan kusini.
Katika kuadhimisha siku hii ya kimataifa ya huduma za kibinadamu , moja ya nchi ambayo inahitaji kwa hali na mali huduma hizo ni Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, ambayo imeghubikwa na mjangamakubwa matano , kipindupindu, njaa, kutokuwa na uhakika wa chakula, vita nae bola.
Hii leo ni siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu ambapo Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa viongozi ulimwenguni kufanya kila wawezalo kulinda watu walionasa kwenye mizozo.