Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imesema inatiwa hofu kubwa na mauaji ya zaidi ya watu 150 katika maeneo ya Djugu na Mahagi kwenye jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC
Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu iliyotolewa leo Ijumaa inasema mauaji, ubakaji na mifumo mingine ya ukatili inayowalenga jamii ya Wahema katika jimbo la Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC inaweza kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Ijumaa kama kawaida tuna muhtasari wa habari na kubwa zaidi ni mauaji ya watu 117 huko Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kufuatia mapigano kati ya kabila la walendu na wahema, mauaji hayo ni kati ya tarehe 10 na 13 mwezi huu wa Juni.
Hii leo tunaanzia Uganda kuangalia mtazamo wa wananchi katika harakati za kukabili Ebola na mwandishi wetu John Kibego amevinjari Buliisa. Huko DRC nako si shwari walendu na wahema wapigana na maelfu wafurushwa.
Ni jambo la kusitikisha pale ambapo mtu amejiandaa kurejea nyumbani baada ya kuishi ugenini, lakini hatimaye analazimika kukimbia tena kutokana na kukuta makazi yake yamechomwa moto na mali nyingine nyingi zimeharibiwa. Huko ni Ituri, DRC ambako wahema na walendu wanapambana.
Shirika la Umoja w aMataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limeripoti kuwa wakimbizi takribani 4,000 wamekimbilia Uganda kufuatia kushamiri kwa mzozo wa kikabila Jimbo la Ituri na mashambulizi ya vikundi vilivyojihami Jimboni Kivu Kaskazini katika kipindi cha wiki moja tu.