wahamiaji

Idadi kubwa zaidi ya watoto wanaishi nje ya nchi zao kama wakimbizi na wahamiaji:UNICEF Ripoti

  • Waasichana wanahama zaidi kuliko wavulana
  • Watoto wote wa kiume na kike wapo hatarini kufanyiwa vitendo kinyume na haki za binadamu
  • Kuna ongezeko mara 10 la watoto kuvuka mipaka
  • Afghanistan inashika namba 1 kati ya nchi 10 zenye watoto wanaohama nchi zao

Wahamiaji wanaosafirishwa kwa njia haramu wanakabiliwa na madhila makubwa:UNODC

Ripoti ya utafiti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Madawa na Uhalifu UNODC imesema, wahamiaji ambao wanatumia mitandao ya usafirishaji haramu kukimbia nchi zao mara nyingi wanakabiliwa na ukatili wa kupindukia, mateso, ubakaji na kutekwa wakiwa njiani au wanaokoshikiliwa mateka.  

JUNI 28 2021

Uchambuzi wa habari zetu hii leo ambapo kuelekea siku ya mabunge duniani juni 30 tutakuletea mahojiano maalum na mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Neema Lugangira kuhusu nafasi ya bunge kwa umma ikiwemo kuelimisha kuhusu mapambano ya Janga la CORONA. 

Sauti -

Zaidi ya Wananchi wa Venezuela Milioni 5.6 waikimbia nchi yao

Venezuela, ni moja ya Mataifa ambayo wananchi wake wanakimbia kwa wingi na kwenda kuomba hifadhi mataifa mengine ambapo takwimu za hivi karibuni zinaonesha takribani robo ya wananchi wake wamekimbia hali ambayo imefanya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,

Sauti -
2'57"

Niko hai, lakini nahisi nimekufa:Mhamiaji aliyenusurika kifo na Kapoteza watoto 3 baharini 

"Nimepoteza kila kitu," anasema Misrah, mwanamke mhamiaji akijitahidi kusimulia tukio la kutisha mno  la kushuhudia vifo vya watoto wake watatu baharini 

Takriban Wakimbizi 300,000 wapata maambukizi ya virusi vya Corona mwaka 2020

Takriban wakimbizi 300,000 kutoka Mashariki na Pembe ya Afrika, wamepata maambukizi ya virusi vya Corona au COVID-19 kwa mwaka 2020. Idadi hiyo imetajwa kwenye ripoti kuu ya mwaka 2020 ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, kwa bara la Afrika iliyotolewa wiki hii.

Hadithi ya Sakina: safari yake kuanzia kuwa mjane barubaru hadi kuwa mfanyakazi anayejiamini 

Ukosefu wa usawa wa kijinsia huongezeka katika hali za mizozo. Wanawake wameathirika kwa kiasi kikubwa katika suala la usalama wa kibinafsi, upatikanaji wa ajira, rasilimali na huduma za msingi katika mazingira dhaifu, yenye migogoro.  

Watoto 275 wanajikuta  Mexico kila siku wakisubiri kuingia Marekani:UNICEF 

Tangu kuanza kwa mwaka 2021 idadi ya watoto wahamiaji wanaowasili Mexico wakisubiri kuingia nchini Marekani imeongezeka kwa kasi kutoka watoto 380 hadi karibu watoto 3500 amesema mkurugenzi wa kanda ya Amerika Kusini na Caribbea wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF.

Tunahitaji fursa ya kuwafikia haraka wahamiaji walioathirika na moto Yemen:IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limetoa wito wa kupewa fursa ya haraka ya kibinadamu kwenye kituo cha mahabusu cha wahamiaji kwenye mji mkuu wa Yemen,  Sana'a ambako moto mkubwa umeripotiwa kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa mwishoni mwa wiki.

Wahamiaji lazima wajumuishwe katika mipango ya chanjo ya COVID-19

Wataalam wa masuala ya haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa, Afrika, Ulaya na muungano wa mfumo wa haki za binadamu Marekani wametoa mwongozo mpya ukitaka lazima wahamiaji wote wajumuishwe katika programu za jancho dhidi ya corona au COVID-19.