wahamiaji

Uhamiaji sio shida Afrika la msingi kutovunja sheria- Rais Nyusi

Suala la uhamiaji likiendelea kuibua vuta nikuvute, Msumbiji imesema kuwa la msingi ni watu kufuata sheria kwani uhamiaji umekuwepo na utaendelea kuwepo.

Colombia inakabiliwa na janga kubwa:WFP

Colombia inakabiliwa na zahma kubwa wakati huu ambapo maelfu ya raia wa Venezuela wanaendelea kumiminika nchini humo kutokana na ukosefu wa chakula na mahitani mengine ya msingi nchini mwao.

Wahalifu Libya msituchafulie jina:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia  wakimbizi la UNHCR, limetoa wito kwa serikali nchini Libya kuchukua hatua madhubuti dhidi ya wahalifu wanaowalenga  wakimbizi na wahamiaji wakati kukiwa na taarifa za kuwa wasafirishaji haramu  wa binadamu hujifanya kama wafanyakazi wa UNHCR.

 

Machafuko Tripoli yatishia uhai wa wahamiaji na wakimbizi

Machafuko yanayoendelea mjini Tripoli Libya, yamefanya hali kuwa tete kwa maelfu ya watu, wakiwemo wakimbizi na wahamiaji. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa wito wa kukomeshwa mara moja machafuko hayo na kuhakikisha usalama wa raia.

Sauti -