wahamiaji

Watu 100 wafa maji Mediteranea

Bahari ya Mediteranea yazidi 'kumeza' watu, manusura wasimulia walivyopata kiwewe.

Mikakati yoyote kwa wahamiaji Ulaya izingatie haki za watoto- UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesihi Muungano wa Ulaya, EU,  na wanachama wake kuchukua hatua thabiti, za pamoja na za wakati il kuokoa Maisha ya watoto wakimbizi na wahamiaji kabla hawajaingia barani Ulaya.

Taarifa za wahamiaji kutelekezwa jangwani zinasikitisha: IOM

Si haki kwa wahamiaji ambao ni pamoja na kina mama wajawazito na watoto kutelekezwa peke yao bila chakula wala maji au kutarajiwa wataweza kutembea kwa miguu maili kadha katika joto kali wakitafuta usalama jangwani.

Idadi ya wahamiaji waingiao Ulaya kupitia Mediteranea yapungua- IOM

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa-IOM linasema idadi ya wahamiaji na wakimbizi waliovuka bahari ya Mediteranea mwaka huu wa 2018 sambamba na wale waliokufa maji imepungua ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Watoto hawapaswi kutenganishwa na familia licha ya hali ya uhamiaji-UNICEF

Taarifa ya kwamba watoto wakiwemo wachanga wanatenganishwa na wazazi wao wakati wanatafuta usalama nchini Marekani zinaumiza moyo, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.

19 Juni 2018

Katika jarida la habari hii leo Assumpta Massoi anaangazia.

Sauti -
11'20"

Watoto milioni 30 waliotawanywa na vita wanahitaji kulindwa, na pia suluhu ya kudumu:UNICEF

Takribani watoto milioni 30 waliotawanywa na vita duniani wanahitaji ulinzi sasa na suluhu endelevu na ya kudumu kwa ajili ya mustakbali wao.

Haki za watoto wakimbizi na wahamiaji ni suala la kanuni: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametetea haki za watoto wakimbizi na wahamiaji akisema ni suala la kuzingatia kanuni za haki za binadamu bila kuisota kidole Marekani.

Chondechonde wapokeeni wahamiaji waliokwama melini Mediterranea UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi duniani UNHCR limeziomba serikali husika  kuwakubalia mamia ya watu ambao wamekwama katika bahari ya Mediterani wakiwa ndani ya meli ya  the Aquarius kuingia nchini mwao.

Tuna hofu kubwa baada ya wahamiaji 100 kufa maji Tunisia:IOM

Wahamiaji takriban 100 wamekufa maji, 68 kunusurika na wengine hawajulikani waliko baada ya boti yao kuzama mwambao wa Kerkennah-Sfax nchini Tunisia mwishoni mwa wiki.