wahamiaji

IOM yasaidia kuwarejesha Ethiopia wahamiaji 100 Kutoka Yemen

Raia 101 wa Ethiopia waliokuwa wahamiaji nchini Yemen wameondoka kwa hiyari kwa msaada wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM na kurejea nyumbani kupitia bandari ya Hudaydah.

Algeria acheni kuwatimua kwa pamoja wahamiaji:UN

Umoja wa Mataifa leo umetoa wito kwa serikali ya Algeria kusitisha vitendo vya kuwafukuza kwa pamoja wahamiaji hususani kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ingawa idadi kamili ya waliotimuliwa haijajulikana inaaminika ni maelfu ya wahamiaji.

Maboya chakavu sasa yawa mabegi ya gharama

Maboya chakavu yaliyotumika kuwaokoa na kuwasafirisha wakimbizi na wahamiaji kwenye bahari ya mediterranea sasa yawa na thamani kubwa baada ya kutumika kutengenezea mabegi ya gharama ya kubeba mgongoni.

Sauti -
1'20"

Maboya chakavu yageuzwa mabegi ya gharama

Maboya yamekuwa yanatumika kusafirishia wakimbizi na wasaka hifadhi. Mara nyingi maboya haya yanapotia nanga huko Ulaya huwa yamechakaa na hivyo kutupwa kiholela. Hivi sasa wasichaan wawili huko Ujerumani wamegeuza taka hizo kuwa bidhaa ya aina yake.

IOM na Benki ya Dunia zashirikiana kukwamua wahitaji duniani

IOM na Benki ya Dunia sasa kushirikiana kwenye maeneo  ya kuboresha  ustawi wa kibinadamu.

Lindeni wahamiaji-IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wahamiaji IOM lina wasiwasi kutokana na hali mbaya ya wahamiaji  nchini  Yemen.

 

Wapata kiwewe baharini, UNHCR yaelekeza usaidizi

Nchini Libya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,  UNHCR limeanza awamu ya pili ya kusaidia wakimbizi na wahamiaji waliookolewa mjini Tripoli baada ya kukabiliwa na hali mbaya baharini.