Tuzidishe juhudi kulinda watumishi wa UN-Guterres
Hebu tuimarishe azma yetu ya pamoja na njia za kuwalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakati wakifanya kazi zao bila kuchoka kwa ajili ya amani,maendeleo endelevu na vilevile haki za watu wote, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo.