Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

viwavi jeshi

UN News / Thelma Mwadzaya

Viwavi jeshi vimerejea Afrika Mashariki, FAO kusaidia kuvikabili

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, limetahadharisha kuwa viwavijeshi ambavyo vimeripotiwa kuonekana kwenye mbuga na hifadhi za wanyama nchini Kenya vimerejea.Wadudu hao pia wameonekana kwenye mataifaJirani ya Eritrea, Sudan Kusini,Ethiopia, Somalia na Uganda. Ifahamike kuwa mwaka 2016 viwavijeshi vilionekana kwenye mataifa 6 pekee barani Afrika.Viwavijeshi vina uwezo wa kuvamia na kukomba mazao ya mahindi, ngano, mtama, shayiri na nyasi. Kwa undani zaidi wa juhudi hizo ungana na mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya katika Makala hii.

Sauti
3'48"
Shamba la mahindi lililoshambuliwa na viwavi jeshi Malawi. Sasa vyahamia Bara Hindi.
FAO/Rachel Nandalenga

Viwavi jeshi vimerejea Afrika Mashariki, FAO kusaidia kuvikabili

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO,limetahadharisha kuwa viwavijeshi ambavyo vimeripotiwa kuonekana kwenye mbuga na hifadhi za wanyama nchini Kenya vimerejea. Wadudu hao pia wameonekana kwenye mataifa jirani ya Eritrea, Sudan Kusini, Ethiopia, Somalia na Uganda. Ifahamike kuwa mwaka 2016 viwavijeshi vilionekana kwenye mataifa 6 pekee barani Afrika. Viwavijeshi vina uwezo wa kuvamia na kukomba mazao ya mahindi, ngano, mtama, shayiri na nyasi. 

Viwavi jeshi katika  mmea wa mahindi Lesotho
FAO/Lesotho/Lechoko Noko

Apu ya Nuru kumkomboa mkulima Afrika- FAO

Apu iliyopatiwa jina la Nuru na ambayo inazungumza lugha tatu; Kiswahili, Kifaransa na Twi  imezinduliwa na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa lengo la kuwezesha mkulima kubaini aina mpya ya viwavijeshi ambavyo ni tishio kwa mazao barani Afrika. 

Sauti
1'41"