Maisha magumu yanawafanya wananchi kukimbia makazi yao: IOM
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema wananchi wengi wa Tunisia hivi sasa wanakabiliwa na machaguo magumu ya kubaki ndani ya nchi yao na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha na uhaba wa chakula au kukimbia nje ya nchi yao na kutojua nini kitatokea huko waendako.