Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO amezuru maeneo yaliyoathirika vibaya na kimbunga katika visiwa vya Bahama na kutoa wito wa msaada zaidi wa kibinadamu kwa waathirika wa kimbunga hicho.
Tunahitaji kuhakikisha tunakomesha mabadiliko ya tabianchi amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baada ya kurejea kutoka Abaco katika visiwa vya Bahama ambako kumeathirika sana na kimbinga doriani.
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Martin Griffiths amesema anatiwa hofu kubwa kuhusu mashambulio yaliyofanywa na ndege isiyo na rubani au drine katika vituo viwili vya mafuta kwenye Ufalme wa Saudi Arabia.
Viongozi wa dunia watakaohudhuria mkutano unaokuja wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wametakiwa kuja wamejizatiti sio na hotuba bali mipango ya kufikia malengo ya kupunguza hewa ukaa na kuimarisha mnepo dhidi ya changamoto hiyo ya kimataifa.
Kimbunga Dorian kikiendelea kuleta madhara huko visiwa vya Bahamas, ripoti zinasema kwamba watu watano wamethibitishwa kufariki dunia huku mashirika ya Umoja wa Mataif ana wadau wakiwa wamepeleka watendaji wake kufanya tathmini ya uharibifu.