Viroboto

Mlipuko wa Bubonic unahatarisha maisha ya watoto Congo DRC: UNICEF

Kuibuka tena kwa ugonjwa wa Bubonic unaosambazwa na viroboto kutoka kwa wanyama kama panya na nguchiro kwenda kwa binadamu baada ya kuwauma na kisha binadamu aliyeambukizwa kuweza kuambukiza binadamu mwingine, kunaweka maisha ya watoto na vijana hatarini, katika jimbo la Ituri Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)  limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.