Njombe wafurahia usaidizi wa UN
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo kutoka Uingereza, Marekani na Sweden na serikali ya Tanzania linajitahidid kutekeleza mpango wa kunusuru kaya masikini (PSSN) kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), ambao kwa sasa umefikia takriban kaya milioni 1.1 wenye umasikini uliokithiri nchini humo...