vijana

Tukiwawezesha vijana watakuwa waunda ajira na sio wasaka ajira:UNIDO 

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO limesema vijana wanachokihitaji ni nyenzo, mbinu na muongozo ili kujenga kesho wanayoihitaji na hasa kupitia ujasiriliamali. Maelezo John Kibego yanafafanua

Mienendo ya ujanani inavyoweza kuwa baraka au balaa uzeeni -Sehemu ya kwanza

Mienendo ya mtu katika ujana wake hutoa matunda yake au machungu wakati wa uzee, anasema mzee mmoja nchini Uganda aitwaye Peter Semiga ambaye sasa ametimiza umri wa miaka 80. 

Sauti -
3'31"

Vijana Nyeri Kenya waona nuru ya maisha kupitia usindikaji wa ndizi 

Chukua vijana wajasiriamali, wapatie vifaa vya kisasa na mafunzo basi utakuwa umebadilisha maisha si ya kwao tu bali na jamii zao ,na hicho ndio kilichotokea huko kaunti ya Nyeri nchini Kenya baada ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya kushikana mikono na kunasua vijana ambao walikuwa kidoto wakate tamaa.

Taka za mferejini Haiti zageuzwa kazi za sanaa na kuibua vipaji vya vijana waliokata tamaa.

Kitongoji cha Cité Soleil, kwenye mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, unatambulika kwa maisha duni, umaskini uliokithiri na ghasia za kila uchao. Vijana wamekata tamaa!

Sauti -
3'42"

Vijana Uganda wakaribisha sheria ya kugombea chini ya umri wa miaka 30.

Kwa miaka 25 ya katiba ya Jamhuri ya Uganda, vijana walio chini ya umri wa miaka 30 wamekuwa wakisaka fursa ya kukubaliwa kugombea nafasi mbalimbali za kisiasa katika serikali za mitaa kutokana na vizuizi vya sheria za uchaguzi.

Sauti -
3'46"

Somalia vijana wakutana kujadiliana kuhusu ushiriki wao kuiendeleza nchi yao 

Vijana wa Somalia wametakiwa kuwa waleta mabadiliko na kushiriki kikamilifu katika siasa, upatanishi, kuleta amani, uchaguzi na juhudi zinazoendelea za kusaidia kuendeleza nchi yao. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Sauti -
1'55"

Vijana wa Somalia wakutana kujadiliana kuhusu ushiriki wao kuiendeleza nchi yao 

Vijana wa Somalia wametakiwa kuwa waleta mabadiliko na kushiriki kikamilifu katika siasa, upatanishi, kuleta amani, uchaguzi na juhudi zinazoendelea za kusaidia kuendeleza nchi yao.

Baada ya miaka 75 tumepiga hatua kubwa na tuna ya kujivunia, lakini safari bado ni ndefu:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema Umoja wa Mataifa una mengi ya kujivunia baada ya kupiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake miaka 75 iliyopita, lakini bado safari ni ndefu inayohitaji mshikamano wa kimataifa na utashi wa hali ya juu wa kisiasa kukabili changamoto zinazokikikumba kizazi hiki na vijavyo.

Heko Rwanda kwa uzinduzi wa Gen U, ni hatua kubwa:UNICEF 

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeipongeza serikali ya Rwanda na watu wake kwa kuzindua mkakati wa kikazi kisicho na ukomo au Generation Unlimited (Gen U).  

Kiwanda cha chaki Ikungi Singida ni matunda ya mafunzo niliyopata Restless Development- Simon

Nchini Tanzania, shirika la kiraia la Restless Development limekuwa mstari wa  mbele kuona vijana wanapata stadi mbali mbali muhimu ili hatimaye siyo tu wawe viongozi kwenye jamii zao bali pia waweze kushiriki shughuli za ujasiriamali na kunusuru vijana wenzao kutoka katika lindi la  Umaskini.

Sauti -
2'23"