vijana

Teknolojia inasaidia vijana kusambaza bidhaa wanazotengeneza

Nchini Tanzania vijana wajasiriamali katika mkoa wa Singida wameitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEHAMA kama njia mojawapo ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDG hususan kipengele cha teknolojia cha lengo namba 17 la kuimarisha mbinu za utekelezaji wa malengo na kuchochea ubia wa kimataifa.

Mjadala Mkuu wa ngazi za juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa waanza rasmi

Mjadala Mkuu wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA76 leo umeng’oa nanga rasmi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani ukifanyika moja kwa moja na pia kupitia mtandaoni ukiwaleta pamoja nchi 193 wanachama wa Umoja huo.

Vijana ni nguzo muhimu kwenye kulinda amani:Guterres 

Katika kuelekea siku ya walinda amani dunaini Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mchango wa vijana katika kudumisha amani ni mkubwa na amani haiwezi kupatikana endapo hawatoshirikishwa.

Masomo shuleni na vyuoni yaendane na hali halisi kwenye jamii – Benki Ya Dunia Ghana

Nchini Ghana Benki ya dunia pamoja na vijana wamebaini kuwa kwa kiasi kikubwa masomo yanayofundishwa shuleni na vyuoni hayamwezeshi kijana kujikimu na maisha pindi anapohitimu masomo na mara nyingi vijana kujikuta wakifanya shughuli ambazo hata hawakuzisomea.

Tukiwawezesha vijana watakuwa waunda ajira na sio wasaka ajira:UNIDO 

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO limesema vijana wanachokihitaji ni nyenzo, mbinu na muongozo ili kujenga kesho wanayoihitaji na hasa kupitia ujasiriliamali. Maelezo John Kibego yanafafanua

Vijana Nyeri Kenya waona nuru ya maisha kupitia usindikaji wa ndizi 

Chukua vijana wajasiriamali, wapatie vifaa vya kisasa na mafunzo basi utakuwa umebadilisha maisha si ya kwao tu bali na jamii zao ,na hicho ndio kilichotokea huko kaunti ya Nyeri nchini Kenya baada ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Kenya kushikana mikono na kunasua vijana ambao walikuwa kidoto wakate tamaa.