Victoria Tauli-Corpuz

Congo tekelezeni kimatendo sheria ya kulinda watu wa asili- Mtaalam

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa jamii za asili, Victoria Tauli-Corpuz amehitimisha ziara yake ya siku  11 nchini Jamhuri ya Congo na kusisitiza umuhimu wa serikali kutekeleza kwa vitendo sheria ya kusongesha haki za jamii hiyo.

Wataalam wa UN watoa wito serikali ya Ufilipino kusitisha mashambulizi dhidi ya Victoria Tauli-Corpuz

Madai ya uongo yanayoelekezwa dhidi ya mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na serikali ya nchi yake Ufilipino hayana mashiko kiukweli au kisheria na ni lazima yasitishwe haraka iwezekanavyo imesema taarifa ya wataalam wenzake iliyotolewa leo Jumatano na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR mjini Geneva, Uswisi

Mashambulio haya ni lazima yajibiwe- Zeid

Kamishna mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein, amekemea  hatua za utawala wa Ufilipino za kumuweka katika orodha ya magaidi, muwakilishi  maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu asili, Victoria Tauli-Corpuz na kusema  kitendo hicho  hakikubaliki na kusema ni lazima lijibiwe.

 

Sauti -
1'29"

Zeid aikemea Ufilipino kumuorodheshwa mwanarakati wa haki kama gaidi

Kamishna mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein amekemea  hatua za utawala wa Ufilipino za kumuweka katika orodha ya magaidi, uwakilishi  maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za watu asili, Victoria Tauli-Corpuz.