Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uvuvi wa asili

UN Tanzania

FISH4ACP wahifadhi mazingira ya Ziwa Tanganyika nchini Tanzania

Mkoani Kigoma nchini Tanzania wavuvi katika ziwa Tanganyika waliopatiwa mafunzo na FAO Tanzania kupitia mradi wake wa Fish4ACP sasa wana mtazamo tofauti na ule waliokuwa nao kabla ya kupatiwa mafunzo kwa kuzingatia kuwa ukosefuwa elimu ya uhifadhi wa mazingira huleta madhara katika nyanja mbalimbali, madhalani baadhi ya wavuvi wanaotumia mbinu za asili bila kujali mazingira wanaweza kusababisha kupungua kwa viumbe maji na hata kukosekana kwa mazao ya uvuvi.  Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM anafafanua zaidi.

Sauti
3'17"