Utumikishwaji kwenye kazi na kwenye ndoa vyaongezeka
Watu milioni 50 walikuwa wakiishi katika utumwa wa kisasa mwaka jana 2021, kwa mujibu Ripoti ya hivi karibuni ya makadirio ya utumwa wa kisasa duniani ambayo imetolewa na shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa, ILO, Wakfu wa Walk Free na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Taarifa inayowasilishwa na Anold Kayanda ina maelezo zaidi.