Chuja:

utafiti

UNICEF/Shehzad Noorani

WHO:Huduma za afya zimevurugwa katika asilimia 90 ya nchi wakati wa COVID-19

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, leo limechapisha utafiti wake wa kwanza wa athari za janga la corona au COVID-19 kwa mifumo ya afya duniani. Hali ikoje? Loise Wairimu na taarifa zaidi.

Katika utafiti huo uliofanyika na takwimu kukusanywa katika nchi 105 duniani tangu mwezi Machi hadi Juni mwaka huu wa 2020, unaonyesha kuwa takriban asilimia 90 ya nchi hizo huduma zake za afya zimekabiliwa na changamoto huku nchi za kipato cha chini na cha wastani zikiarifu matatizo makubwa zaidi. 

Sauti
1'45"