Skip to main content

Chuja:

Usonji

3 Aprili 2020

ASSUMPTA: Hujambo na karibu kusikiliza jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa mimi ni ASSUMPTA MASSOI nikiwa hapa hapa New York Marekani

 

JINGLE (04”)      

 

ASSUMPTA: Ni Ijumaa  ya April  03 mwaka 2020 na kama ilivyo ada leo ni mada kwa kina ambapo leo tutamsikiliza mtaalamu wa afya upande wa tatizo la usonji akitueleza kinagaubaga kuhusu tatizo hilo.  Kwanza tupate Habari kwa Ufupi, ikiwasilishwa na Grace Kaneiya. 

====================================================

STUDIO: Play Habari kwa UFUPI

 

Sauti
9'58"
UNICEF

Kuwa na mtoto mwenye usonji ni changamoto na COVI-19 imeongeza zaidi

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusiana na tatizo la usonji, Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano na watu wenye tatizo hilo la kiafya hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19.

Nchini Tanzania janga la COVID-19 hata hivyo limetia doa maadhimisho hayo kama anavyoelezea Isaac Maro ambaye pia ni mzazi wa mtoto mwenye usonji.

(SAUTI YA DKT. ISAAC MARO)

Sauti
3'3"

02 APRILI 2020

Katika Jarida la habari hii leo assumpta Massoi anakuletea

-Siku ya uelimishaji kuhusu usonji ikiadhimishwa leo Umoja wa Mataifa umetoa wito kuhakikisha watu hao wanajumuisha katika harakati za kupambana na janga la virusi vya Corona , COVID-19

-Huko nchini Suda Kusini japo bado hakuna mgonjwa yeyote wa virusi vya Corona COVID-19 mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS kwa kushirikiana na serikali wachukua hatua kujikinga ikiwa ni pamoja na kufunga soko kubwa mpkani wa nchi hiyo na DRC

Sauti
12'59"
Mahmood ambaye ana usonji akiwa ameshika herufi P ambayo aliambiwa aitafute kwenye boksi darasani nchini Misri
© UNICEF/Rehab El-Dalil

Janga la COVID-19 linawaweka watu wenye usonji katika hatari kubwa.

Kupitia ujumbe wake maalum kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku ya uelimishaji kuhusu usonji inaadhimishwa kwa kutambua na kusherehekea haki za watu wenye usoni na kwamba “Mwaka huu siku hii inaadhimishwa katikati ya janga la kimataifa la kiafya ambalo hatujawahi kulishuhudia katika maisha yetu, janga ambalo linawaweka watu wenye usonji katika hatari kubwa kutokana na virusi vya Corona na athari zake katika jamii.”