Mvutano wa China na Marekani kibiashara waumiza wananchi wao- UNCTAD
Msemo wa wahenga ya kwamba wapiganapo mafahali wawili ziumiazo ni nyasi, sasa imebainika vinginevyo katika vuta nikuvute ya ushuru kati ya Marekani na China ambapo Umoja wa Mataifa umesema mafahali hao wawili ndio wanaoumia zaidi na wananchi wao.