Ushirikiano wa kimataifa

Jarida 28 Septemba 2021

Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo utasikia shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO na wadau wake wamezindua mkakati wa kwanza wa aina yake wa k

Sauti -
13'46"

Akiwa Urusi Guterres aonya dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi na kudorora kwa uchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameainisha changamoto za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s na kukumbusha umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa kwenye jukwaa la kimataifa la kiuchumi 2019 (SPIEF)  linalofanyika huko St. Petersburg nchini Urusi.

Kwa wananchi wa kawaida vitendo ni bora kuliko maneno au hotuba:Espinosa

Maneno matupu na hotuba bila vitendo halisi na hatua zinazoonekana katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu, havina faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Hayo yamesemwa leo na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa ufunguzi wa hafla ya maadhimisho ya kwanza ya siku ya ushirikiano wa kimataifa na amani kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New york Marekani.

Ushirikiano wa kimataifa ni nguzo kwa dunia na kila mmoja:Guterres

Ushirikiano wa kimataifa na diplomasia vimethibitisha kuwa na faida na huduma muhimu kwa watu wote duniani kuanzia masuala ya utekelezaji wa sheria za kimataifa, usawa wa kijinsia, ulinzi wa mazingira, hadi kuzuia uzalishaji wa silaha za maangamizi na hata magonjwa hatari duniani, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa maadhimisho ya kwanza ya kimataifa hii leo ya “siku ya ushirikiano wa kimataifa na diplomasia kwa ajili ya amani”

Guterres:Tunahitaji ushirikiano wa kimataifa sasa kuliko wakati mwingine wowote

Ushirikiano wa kimataifa unahitajika duniani kuliko wakati mwingine wowote ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikibali dunia hivi sasa kwa pamoja.

Sauti -
3'18"

Tunahitaji ushirikiano wa kimataifa sasa kuliko wakati mwingine wowote:Guterres

Ushirikiano wa kimataifa unahitajika duniani kuliko wakati mwingine wowote ili kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikibali dunia hivi sasa kwa pamoja.