Mabadiliko ya kisiasa ya mamlaka nchini Sudan yana athari za wazi kuhusu hali jimboni Darfur, amesema Mwakilishi maalum wa Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika, jimboni humo, UNAMID.
Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Ursula Mueller yuko ziarani nchini Burkina Faso ambakoamesema mahitaji ya kibinadamu yameongezeka kwa kiwango cha juu tangu mwezi Juni mwaka jana 2018 na katika miezi ya hivi karibuni.