Ripoti 3 zaonesha athari wanazokabiliana nazo watoto wa Rohinghya
Utapiamlo uliokithiri, upungufu wa damu na kipindupindu vyawakumba watoto wadogo wa kabila la Rhohingya waliokimbilia nchini Bangladesh.
Ripoti tatu maalum za shirika la kuhudumia watoto ulimwenguni UNICEF zinasema katika kila watoto 5, wawili kati yao wanaugua kipindupindu, na mmoja kati ya 5 ana utapiamlo uliokithiri huku mmoja kati ya 2 ana upungufu wa damu.
Mwakilishi wa UNICEF Bangladesh Edouard Beigbeder, ametaka juhudi za haraka zifanyike kuokoa watoto hao
(Sauti ya Edouard Beigbeder)